Welcome to dotSUB!
Any Video Any Language
Here you can view, upload, transcribe and translate any video into any language. To create your own subtitles, click the button below and register.
Enterprise Solutions
dotSUB's Enterprise Solutions are a cost-effective platform for managing high-quality subtitles at scale, deploying them to video players and mobile devices, and providing interactive transcripts for enhanced SEO.
Transcript for AMINAS DREAM
Ndoto yake Amina imebaki kuwa kama kitendawili kwa wengi anayeweza kuihadhithia kutoka rohoni si mwengine ila yeye mwenyewe. Ilikuwako mwezi wa kumi na mbili Jumapili nilipokuwa nikisubiri mtihani wa indeksi namba yani keshoyake Jumatatu tulikuwa tutafanya mtihani. Kwasababu nilifichwa nikielezewa zaidi kuwa alikuwa anaumwa na kichwa tu. Hata hivyo nafsini mwangu mlikuwa na maswali nikijiuliza ya kuwa tokea lini matron akaambatana na mwanafunzi kwenda nyumbani kwao ilihali mzazi wake yuaumwa tu na kichwa. Nilipokuwa nikielekea huko nyumbani nilimwambia rafiki yangu ya kwamba mimi naenda nyumbani lakini ukweli ni kwamba kama baba hakufa mama ndo amekufa na kufika nyumbani watu walikimbia mbio kuja kunikumbatia. Kina dada na kina kaka, wote wakiniambia hatuna baba. Nilipelekwa mpaka chumbani kwa baba kufika nikampata baba kitandanii ihi mmhi. Sikuamini macho yangu lakini haki baba alikuwa ameshakufa. Hata hivyo ndugu zangu hakuna hata mmoja ambaye ana kazi ya kuajiriwa. Ni vibarua tu na hivyo basi mimi ndiyo nimekuwa kama nyota ya jamii. Ninajitahidi kwani lengo langu ni kuwa jonalisti na nikiangalia hivi nyota yangu iko karibu kutimia kwani nilikuwa mwanamemba wa video projecti Moyeni na saa hii naendelea na YETAM. Mungu yuko pamoja nami na baba pia yuaniangalia popote alipo.

